The Moroccan Maradona (Maradona wa Moroko)




 Ismael Saibari Ben El Basra, alizaliwa tarehe 28 Januari, mwaka wa 2001, jijini Terassa, Uhispania, kutoka Kwa wazazi wenye asili ya Moroko.Ana nfugu wawili, Akram na Adam Saibari. Akiwa miaka 6 hivi, familia yake uliamua waende kule ubelgiji kisa na maana, ni kwamba, uchumi wa Uhispania ulikuwa umezororata na kule ndipo safari yake ya soka ilipoanza.



Alianza Kwa kuchezea akademia zilizo tajika kule ubelgiji. Baadhi ya zile akademia ni kama;

Beerschot( alikoanza)
Anderlecht
KV Mechelen
Genk

Baadaye, alijiunga na akademia kuu ya klabu ya PSV Eindhoven, Jong PSV kabla ya kupewa rasmi nafasi kwenye timu ya kwanza ya PSV, hii ilitendeka kule Julai 29,2020, Kwa mkataba wa miaka mitatu.


PSV

Mechi yake ya kwanza akiitumikia klabu hii kwenye ligi kuu, Uholanzi, ulikuwa dhidi ya ADO Den Haag,ambapo alibadilishana kipindi cha pili na gwiji wa zamani wa Ujerumani, Mario Gotze.Mechi hiyo , klabu yake ilishinda mabao manne Kwa Moja.Bao lake la kwanza ulikuwa dhidi ya Vitesse, wakishinda Kwa mabao matatu Kwa Moja.Mwezi uo huo, walicheza kwenye mechi ya kufuzu klabu bingwa bara ulaya, (uefa champions league). Walijizatiti na kutitiga Rangers kutoka uscotii, hivyo kufuzu kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Mwaka wa 2023,aliongeza mkataba wa miaka mitano na 29 Novemba, walicheza dhidi ya Sevilla na kushinda wakiwa ugenini, mabao tatu Kwa mbili.

Kuanzia msimu wa 2023/24, walianza kumpa wakati mwingi wa kuweza kucheza.Aliipata hattrick yake ya kwanza dhidi ya Feyenoord. 

Msimu wa mwaka wa 2025/26, kinda huyu alibobea katika tasnia yake.Alifanikiwa kuchezea mechi44 ambapo alipiga mabao 15 na assist 13.

Msimu huu ndipo alipewa tuzo ya mchezaji Bora wa msimu huo.

Kwa taarifa za hivi karibuni, inaaaminika kwamba Saibari ameweza kusaini mkataba na Bayern Munich, kutoka Ujerumani, wa miaka mitano Kwa paundi millioni 50, sawa na takriban billioni Saba za Kenya.

Kimataifa, tangu ujana wake hadi sasa, ameishi kuitumikia timu ya taifa ya Moroko, licha ya nafasi nyingi alizopata kuchezea mataifa mengine na hata mengine, yeye mwenyewe akikiri kwamba mameneja wengine walikuwa wakimsusia kwamba wanahitaji huduma yake kwenye timu hizo za taifa. Baadhi ya makocha ambapo Saibari anataja ni kama kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez, mwaka wa 2022, akitaka kumshinikiza achezee Ubelgiji,lakini Saibari akikiri alikataa hivyo.

Licha ya haya, amekua nguzo kwenye timu ya taifa ya Moroko, akisaidia wao kutwaa ubingwa wa kombe la mataifa barani Afrika Kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 23.Alihusishwa pia katika kombe la mataifa barani Afrika mwaka Jana, akiwakilisha nchi yake.

Katika kombe la Dunia ambayo inaendelea Kwa sasa, ameweza kuifikisha nchi yake hadi katika hatua ya robo fainali ambapo waliondolewa na ufaransa mabao mawili Kwa Moja.Ameeandikisha remodi kadhaa, baadhi ni:

Kuwa mchezaji wa pili, baada ya Mohammed Salah wa Misri, kutoka barani Afrika, kutinga mabao Kwa mechi mbili mfululizo.
Kuwa mchezaji pekee kutoka Afrika kufunga katika mechi tatu mfululizo.
Ingawaje, baadaye alipata jeraha na hivyo, kukosa mechi kadhaa.

Anajulikana na wengine kama " Moroccan Maradona" Kwa sababu ya ueledi wake uwanjani, unaosahibiana kw ukaribu na mchezaji wa zamani wa Argentina, Marehemu Maradona.



Kwa sasa wadadisi wengine wanatabiri ataimarisha kikosi ya Bayern katika Safy ya kati Zaidi.




Saibari baada ya Kusaini mkataba na Bayern Munich







Saibari kwenye mechi yake ya kwanza pale PSV dhidi ya ADO Den Haag.







 













 










Comments

Popular posts from this blog

South African football

AFRICAN FOOTBALL