MANZUR OKWARO
Suleiman Manzur alizaliwa Machi 23, 2006 katika Kaunti ya Bungoma nchini Kenya.Alipohitimu miaka 7, aljjiunga na shule ya msingi ya St. Joseph's pale Webuye, iliyomilikiwa na kanisa la kikatoliki.Baada ya masomo ya shule ya msingi, alijiunga na shule ya sekondari ya St. Anthony Kitale lakini kabla ya hapo, ananukuliwa katika mtandao akikiri kwamba alienda majaribio katika shule kadhaa mojawapo ikiwa St Peters kule Mumias. Anaendelea akisema kwamba, alisaidiwa na Msamaria mwema kwa jina la Wangaya ili kuenda majaribio kule Kitale, alikosoma shule ya upili.Mama yake kirasmi anajulikana kama Caroline Mtila.
St Anthony na Rainbow FC
Akiwa pale Kitale, aliweza kushiriki mashindano kadhaa ya pale shuleni kama COPA COCACOLA na mengine na hata kuitwa katika timu ya taifa kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka kumi na minane.
![]() |
| Manzur akiwa St Anthony Kitale |
Baada ya kukamilisha kidato cha nne, alifanikiwa kijiunga na klabu ya Rainbow, ambayo kwa sasa ni Glorions na kukutana na wenzake kama Tyron Kariuki na Ryan Ogam.Akiwa Rainbow, inakisiwa kwamba alienda majaribio kule Uswidi na klabu ambayo haijulikani kiuwazi. Mwaka wa 2023, yeye pamoja na Linus Munyao, walibahatika kujiunga na Nantes, timu ya pili ili kufanya majaribio kule Ufaransa.
KCB
Alijiunga na Wanabenki baada ya kuonyesha umahiri katika mashindano ya cecafa kwa vijana wasiozidi miaka kumi na minane.Alijiunga na KCB kutoka Rainbow na akiwa KCB, ndipo akaitwa katika timu ya taifa kwa vijana wasiozidi miaka ishirini na akashiriki katika kombe la mataifa ya Afrika Kwa vijana wasiozidi miaka ishirini kule Misri.Kikosi ile, ilikuwa pamoja na Aldrine Kibet na Amos Wanjala kama nahodha.
![]() |
| Manzur akiwa KCB RFC |
NAIROBI UNITED
Manzur aljiunga na Nairobi United baada ya wao kupandishwa daraja kutoka kwenye ligi ya NSL msimu wa 2024/25. Alicheza nao msimu wa 2025/26.
![]() |
| Manzur akijiunga na Nairobi United |
Akiwa huku, alipata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kimataifa ya vilabu ya Afrika, baada ya kushinda kombe la Mozzart bet dhidi ya GorMahia. Alifanikiwa pamoja na klabu yake hiyo baada ya kufuzu katika kombe la mashirikisho ya Afrika( CAF Confederation cup) , katika hatua ya makundi.Ndipo baadaye akaitwa Stade de Reims kule Ufaransa ambapo yupo hadi sasa.
![]() |
| Manzur akiwa Stade de Reims, Ufaransa |
Mafanikio yake pamoja na Ryan Ogam na pia Kibet, ni ishara tosha kwamba talanta ipo Kenya.





Comments
Post a Comment